Kanisa
la Prophetic & Biblical International Ministry (PBIM) Iringa limetoa msaada
wa chakula na vifaa vya shule wajane na watoto yatima zaidi ya 200 kupitia
ibada maalum iliyofanyika kanisani hapo.
Pia,
walikabidhi msaada huo kwenye Shule ya Watoto wasiosikia ya Mtwivila, Manispaa
ya Iringa.
Nabii
wa kanisa hilo, Bruno Massae amesema lengo la msaada huo ni kupanda mbegu ya
upenzi kwa jamii ambayo inapaswa kuwajali na kuwasaidia wahitaji kama wajane na
watoto yatima.
Akizungumza
kwenye ibada hiyo, Diwani wa Kata ya Mkimbizi, Eliud Mvela amelipongeza kanisa
hilo kwa utaratibu wake wa kuisaidia jamii ya watu wasiojiweza kila mwaka.
“Niombe
taasisi nyingine kwenye kata hii kuiga huu mfano, tuwasaidie wahitaji na huo
ndio upendo,” amesema Mvella.
Diwani wa kata ya Mbimbizi, Eliud Mvella ambaye alikuwa mgeni rasmi
Prophet Bruno Massae akihubiri kanisani hapo